Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2017
11....kama kawa tujuavyo, kuna masikabila mvua, pia zasaidiapo, biasharakuzijua, wengi wapata kipato, wengi tumeshuhudia, simu zatusaidia, Sisi ndo twaziharibu, ....12....Wasiliano rahisisha, nje na  ndani pia, umoja zimedumisha, wote kuwa familia, mengi imebainisha, mazuri mabaya pia, sisi ndo twaziharibu, simu zatusaidia. . . . 13. . . . Nukuu twazitafuta, ziloandikwa kwa kina, Dalihini kuzipata, mengi yameambatana, walimu kuzifumbata, zote kuzishikamana, simu zatusaidia, Sisi ndo twaziharibu, . , 14. ..Zapunguza pia muda, wa kuanza tafutana, diradira za ukuda, zapungua kwa sana, Hakuna muda poteza, wafanya mambo mengine, sisi ndo twaziharibu, simu zatusaidia, . ...15. ..Hakuna wa kubabaka, ukweli wajulikana, japo wametuletea, ila zinatupumbaza, mzazi simpe mwana, ukaona wampenda, Hapo unampoteza, bila mwnywe kujua, ....KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA NAENDELEA KUWAKARIBISHA USHAURI, MAONI NAHITAJI
Jamani wanawake tusaidianeni, tupeane kampani support, tunaweza tunaweza, wanaume wasituchezee, jamani mi nashangaa wanawake t unalia kbb ya mapenzi, tunakua kama vile hakuna tunachowaza tunawaza mapenzi tu, mapenzi yenyewe yanatutesa, yanatuliza, mwanaume anayekuliza sio kabisaaa move on maisha yaende, I have

MTOTO WA MAMA /BABA WA KIDIGITALI

SHAIRI HILI NI ZURI SANA LINAONGELEA WAZAZI WA KIDIGITALI NA MALEZI /MAKUZI YA WATOTO, WAZAZI WA SIKU HIZI WAMEJISAHAU SANA KWENYE MALEZI YA WATOTO HII NI HATARI KWA MENGINE TUUNGANE KATIKA SHAIRI HILI, KARIBUNI SANA, ..."""""MTOTO NA MAMA AU BABA WA KIDIGITALI """""1....Mambo yamebadilika,wazazi zama na sasa, Malezi kughafilika, watoto shindwa kuasa, maovu yamefurika, umetuzidi usasa, baba, mama, digitali, mtoto atakuaje? 2....Mama nyonyesha hataki, falaula angejua,Kuja kutahamalaki, mtoto asiyekua, anamkosesha haki, mengine kuyatambua, Mtoto atakuaje? Baba, mama, digitali, ...3....Mtandaoni warusha, sherehe kubwa wafanya, lakini kumnyonyesha, kitu wasichokifanya, mapenzi yasiyokwisha, toto aweze kunyonya,baba, mama, digitali, mtoto atakuaje? 4.....Imani zimewatoka, nguo za wavaa, wajifanya mababaka,elewi yalowajaa, kila siku wanaruka,uzungu usowafaa, mtoto atakuaje? Baba, mama, digital, ..5...Malezi kitu muhimu, msifanye marinara, tuy...
6.......Serikali awamu tano, yasema hapa kazi tu, fanyakazi zembe walo, bado wanazihusudu, hiyo subuhi kuchwayo,Simu ndo kama salamu, wewe ndo uitawale, simu isikutawale. ..7....Zimerahisisha vitu, wanawake wanaume, mtu kutana na mtu, mambo yameenda kume, Mawasiliano butu, yamaliza kila tume,Simu usikutawale, wewe  ndo uitawale, . 8....Zavunja mpaka  ndoa, zachachamua mabosi, zinatia watu doa, sababu ya kuwa ghashi, imani zawaondoa, vichwa havishughulishi, wewe ndo uitawale, simu usikutawale, ..9....Zapoteza ufanisi mambo yanafaitika, wajifanya adinasi, mazuri yanakatika, wanafanya na uasi, mambo yanabadilika,simu isikutawale, wewe ndo uitawale, . 10....Utu wa mtu potea, sababu ya urahisi, watu badilisha namba, simu ndo kiunganishi, ana kwa ana hakuna, moja siku malizana, wewe ndo uitawale, simu isikutawale, ...11....Kama tujuavyo, kuna masika bila mvua, pia zasaidiapo, biashara kuzijua, wengi wapata kipato, tena tumeshuhudia, simu zatusaidia,Sisi ndo twaziharibu, ...12...Wasi...

MITANDAO YA KIJAMII

Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa MwenyeziMungu, lakini pia na kwa wadau wangu wote, ambao wananishauri, na kunipa maoni, kwanza kabisa napenda kuongelea suala la matumizi ya mitandao ya kijamii, limekua tatizo kivipi? naomba tuungane kwa kusoma shairi lifuatalo tuburudike, lakini pia tupate ujumbe kwasababu kama halikugusi wewe moja kwa moja linamgusa ndugu yako au mtu wako wa karibu. ....tuimbe pamoja,,,,1...Whatsup, Facebook, Twitter, insta na napchat, mlahaka vilipata, ghafla ikawa dabali, bila hata ya kusota, wengi walivikumbata, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ..2..Ilianza taratibu, hii teknolojia, dahari ikaharibu, kuja smatifonika, watu wawa kama duku, wawapo mitandaoni, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ...3...zauzwa fulusi ndogo, kila moja amiliki, hata watoto wadogo, zawatia daathari, wanapita kwa mikogo, wazishikapo kwa ari, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ..4...wanafunzi shindwa soma, wabaki kuwa madusa,akili zao zahama,simu zawagusa gusa, wawapo shule ...
HILI NI SHAIRI ZURI SANA KUHUSIAN A NA WATU MUHIMU SANA KATIKA ULIMWENGU WOWOTE ULE, KARIBUNI TUIMBE KWA PAMOJA, 1...TUWAPENDE NA KUWAJALI WALIMU WETU, 1....Honge hongera walimu, kwa kazi mnayofanya, mmeishika hatamu, abadi na siku zote, babatana kuheshimu, baitika hawataki,ualimu ni adhama, apewa kama adia, ...2...japo wanaudharau, walimu fanya adili, wengi wanausahau,lakini tafika dali, watoto wapanda dau, kukua zao akili, ualimu ni adhama, apewa kama adia. ..3....walioko vijijini, hawa watu abtali, wakuta na vizuizi, mazingira kukabili, vigezo haviwakizi,lakini kazi jalili, ualimu ni adhama, apewa kama adia, 4....mwalimu wai kijijini tofauti na mjini, shule mbali  na nyumbani, watembea dahilini, wasipokua makini ,wengi waishia kati, ualimu ni adhama, apewa kama adia, 5...watembea mita nyingi, mashule kuyafikia, wakutana na vigingi, m, waibaaisha kuyatafuta, baadhi ya wananchi,waiba vilotafutwa, ualimu ni adhama, apewa kama adia, 6....shule hazina ofisi,zinazokidhi vigezo, tunafa...
4..Ilikua na karatu, ziara ya kimasomo, mara kwa dakika tatu, vikageuka vilio, walikuepo walimu, pamoja dereva wao, kamwe hatutosahau, watoto wetu wadogo. ..5..wazazi waliobeba, miezi tisa tumboni, watoto waliwabeba, malezi yalo mazuri, fika darasa la saba,hadi yao timia, kamwe hatutosahau ,watoto wetu wadogo..6..hakuna wa kulaumu,katika hili tukio, wengine walishutumu, miliki wa shule hiyo, kilichobaki kutubu, kila moja sala zao, kamwe hatutosahau, watoto wetu wadogo. 7...Nainua macho yangu, niitazame milima, hata na walimu wao, walishindwa kuzuia, kweli ajali tishio, wengi imewachukua, watoto tulowapenda, Allah amewachukua. . . 8...Kulikua na Anord, Rukia naye Gerad, ila yote ni ya God, tubaki kuwaombea,kwa kila aliye moyo, machozi yatamtoka, watoto tulowapenda, Mungu amewachukua. .9.Maisha ya  binadamu, apangaye ni Rabuka, wote sisi tuna hamu, kuishi mpaka kuchoka, japo kifo chatutenga,hatutoacha kuomba, watoto tulowapenda, Mungu amewachukua. .10..Kamwe hatutosahau, Tanzania kwa...

AJALI LUCKY VICENT

HILI NI SHAIRI LA KUWAENZI WATOTO WETU WADOGO ZETU, AMBAO WALIPATA AJALI,....Nikikumbuka nalia, ule mwezi wa tano, watoto walotulia, ilikua tarehe sita, kamwe hatutosahau,tukio lililo baya, watoto tulowapenda,Allah amewachukua. ..2..Nikimkumbuka Junior, pamoja naye Rebeka, waliiga dunia, safari ilotukuka, watatu waliumia, Doreen naye Sadia, kamwe hatutosahau,watoto wetu wadogo, 3..japo yote  ni ya Mungu, ila sisi binadamu tulilia kwa uchungu, kusahau pia ngumu, Allah mgawa mafungu,atajalia wengine, kamwe hatutosahau, watoto wetu wadogo, 4.....

matatizo si kwa ajili ya wanawake

Wanawake wenzangu tupambame, tunaweza kwanza kabisa ni kumtanguliza Mungu, usikubali muda wote unalia, unasinoneka unashindwa kufanya mambo yako kwasababu ya mwanaume , ukiona hana muelekeo songa mbele mi naamini Mungu ndo mpangaji wa kila jambo, ukipambana ukipiga hatua hata mwanaume anakuona mjanja, sio unakaa tu kila kitu unataka uletewe utateseka, sasa kwa nini uteseke na akili unayo, nguvu unayo, na nyie wanaume acheni kutesa wanawake kwasababu tu mmeona hana kazi mpende mtu kwa kila kitu kwa shida na raha usipende kazi kazi hazieleweki......KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA, , , LAKINI KUNA KASHAIRI KAZURII HAPA TUIMBE PAMOJA....

amka acha kulala

Hizi ni qts za kuhamasisha pia "be saying"i can't afford it, "ua brain stops working"by saying "how can I afford it? "Ua brain is put to work. . Usiseme siwezi, kwani walioweza wao wana nini, tuamke wote tuna akili tumejaaliwa na Mungu,      . ...... . . . . . . . . . . No body is superior, no body is inferior, but no body is equal either, people are simply unique, incomparable, you are you, i am i, .........

NYERERE DAY

1.Naabtadi kwa salamu, alikua jemedari, alikua ni mwalimu, na tena ni abtali, wengi walimheshimu, kwa huo weledi, oktoba kumi na nne, siku ya kumkumbuka, 2.alikua na chagaa, watu wasiwe chochole, Afrika kuandaa, isiwe ni kolekole, wazungu walihadaa, hawakua na kongole, oktoba kumi na nne, siku ya kumkumbuka. 3.Alipenda tuwe huru, nchi tuliyozaliwa,mengi hakuyakufuru,kila mtu ajaliwa, walikua msururu, nchi walisimamia,oktoba kumi na nne, siku ya kumkumbuka. 4. Waliona msagunda,nchi yetu panga wao, akatokea kamanda, nyerere wa kambarage, weupe wakamkanda,akawa mtu mshonde, oktoba kumi na nne, siku ya kumkumbuka, .5.walitufanya watumwa,kutupiga kwa silaha, kama vile   walitumwa,ikawa kama karaha, mengi kwetu walifuma, wakijifanya wa raha, oktoba kumi na nne, siku ya kumkumbuka.
11.Shauri pia jirani, uchunguzi ni wa bure, kule kote masikani, hospitali waende, nsemalo niamini, ugonjwa unatibika, saratani ya matiti, ugonjwa unaotisha, .12.Mrs. Mwakyambe, Allah amlaze pema, alitaka apigane, elimu kwa wanawake, gonjwa hili lisione, kuwalinda wanawake, saratani ya matiti, ugonjwa unaotisha.13.maeneo vijijini, elimu bado ni ndogo, wanawake hawajali, wahisi kitu kidogo, ukichelewa chelewa, utakuta mwana si wako, vijijini na mijini, ugonjwa tutokomeze. 14.kama inawezekana,tuanzie mashuleni,Mwanaid naye Anna, walijue kwa undani, wakiujua kwa mana, wataepuka kwa mbali, vijijini na mijini, ugonjwa tutokomeze. 15. Watoto wetu wa kike, tuwalee kipimaji, hatari tusiwaweke,tufanye kama kipaji, apime afya yake, iwe kama mazoea, vijijini na mijini, ugonjwa tutokomeze. . . . KWA LEO TUISHIE HAPO KESHO TENA KUNA SHAIRZURIIII LINAHUSIANA NA TUKIO FULANI LINAKUJA MBELE YETU...ushauri, maoni, www.salimsafina2@gmail.com, 0623398039

SARATANI YA MATITI ELIMU NA JINSI YA KUJIKINGA

Kwanza kabisa naanza, hakuna alo kama mama, yeye ndiye anaanza, dunia kuijakama, japo mengi anawaza, huku Juma huku Rama,saratani ya matiti ugonjwa unaotisha, 2.badiliko chembe hai, mwanadamu,livyoumbwa, anaupenda uhai, ila chembe zaumbua, chembe zaweza badili, katika huko kukua, saratani ya matiti, ugonjwa unaotisha. 3.bada badiliko hayo, ndo zinaleta ugonjwa, ugonjwa kwa jina hilo, unaitwa saratani, wanawake tupendao, wanateseka jamani, saratani ya matiti, ugonjwa unaotisha,4.Na taratibu fulani, na zenyewe zinakua, zinaishi zinakufa, kama vile binadamu, eza tokea athari, fanya zikue zaidi, saratani ya matiti, ugonjwa unaotisha. 5.dalili imojawapo, hutoka kama vivimbe, mara ujigunduapo, ni vyema mstari mbele,watu wengi wahisipo, huogopa kwenda mbele,  saratani ya matiti, ugonjwa unaotisha.6.inaanza taratibu, vingine kama vidonda, watu wengi wapuuza, wakihisi kawaida, hospitali watibu, watu waogopa kwenda, saratani ya matiti, yatutesa wanawake, 7.sidiria tuvaazo, nazo pia sio zuri,...
4.wote tulikua macho, kumtazama kwa hamu,kujua akifanyacho, kuitangaza hatamu, mama kipenzi mtoto, baba alia kwa damu, tulimpata shujaa ,mwenye moyo wa pekee, 5.baba mama msijali, tupo pamoja na nyie, moyo Wauma vikali, nguvu Mungu awatie, mshikamano wa kweli, hili janga lipungue, tulimpata jasiri, mwenye moyo wa pekee. 6.ilikua mwezi nane, kumna mbili kumna saba (2017, Ruzo Boniface Mrima, alionesha u shujaa, mara ni kushika tama, Ruzo kushindwa ibuka, Mungu amlaze pema, yote ni mapenzi yake, .......tuungane wote kumuenzi Ruzo Boniface Mrima
4.Wote tulikua macho, kumtazama kwa hamu, kujua akifanyacho, kuitangaza hatamu, mama kipenzi mtoto, baba alia kwa damu, tulimpata shujaa, mwenye wa pekee.5.baba mama msijali, tupo pamoja na nyie, moyo Wauma vikali, nguvu Mungu awatie, mshikamano wa kweli, hili janga lipungue,tulimpata jasiri,mwenye moyo wa pekee. 6.Likua mwezi wa nane, shirini kumi na saba, Ruzo mtoto wa Mrima, alionesha u shujaa, mara ni kushika tama, Ruzo kushindwa ibuka, tulimpata shujaa, mwenye moyo wa pekee.                             SHAIRI LITAKALOFUATA LITAKUA LINAHUSIKA NA ELIMU JUU YA SARATANI

SHUJAA RUZO

Hili shairi ni zuri sana linaelimsha ni kijana ambaye tulikua naye mwezi wa saba,lakini moyo wake wa pekee leo hatupo naye, ,ukisoma shairi hili utamuelewa vizuri karibuni sana 1.sikitisha familia, na Taifa kijumla, kijana aliyekua, mengi aliyatawala, akataka kuyajua, Dunia yalotawala, tulimpata jasiri , mwenye moyo wa pekee. 2.ndugu wale wa karibu, Mungu awatie nguvu, mmepata majaribu, la muhimu ni kutubu, Tanzania yaabudu salama ilo ajabu, tulimpata shujaa mwenye moyo wa pekee. 3.ila yote ni ya Mungu,kwa kila litokealo, sema sana twakufuru, dhaifu viumbe tulo, ndani ya dakika tatu, akakata yake roho, tulimpata jasiri, mwenye moyo wa pekee ...
Hello wadau wangu hili ni shairi maalumu kwa ajili ya kumuenzi mpendwa wetu,shujaa wetu ambaye alitaka kutuwekea historia wa Tanzania na Dunia kwa ujumla,unahitaji kumjua ni nani karibu tumuenzi kwa pamoja! !!SHUJAA RUZO  1.sikitisha familia, na Taifa kijumla,kijana aliyekua mengi aliyatawala, akataka kuyajua, Dunia yalotawala, tulimpata jasiri, mwenye moyo wa pekee.2.ndugu wale wa karibu Mungu awatie nguvu,mmepata majaribu, la muhimu ni kutubu, Tanzania yaabudu,salama ilo ajabu, tulimpata shujaa mwenye moyo wa pekee. 3.Ila yote ni ya Mungu, kwa kila litokealo, sema sana twakufuru, Dhaifu viumbe tulo, ndani ya dakika tatu, akakata yake roho, tulimpata jasiri, mwenye moyo wa pekee.
Apita huku na kule, wanawake hamasisha, mkubwa yalo ya kale, kujitambua onesha, mazuri waweke mbele, mabaya kuyakomesha ,Rais wa siku zote ,tulomuomba Rabuka. 7.waziri mku Majaliwa, hapa kazi tu jamani, mengi amejaaliwa, mazuri yalo makini, uzembe usotakiwa, kudhibiti asilani, Rais wa siku zote, tulomuomba Rabuka. 8.Fanya kazi mazoea,kwa kila mfanyakazi, leo tumeshuhudia kauli ya hapa kazi, mafisadi waloloea, kufanya kazi ujuzi, Rais wa siku zote, tulomuomba Rabuka.9. Japo mwanzo ni mgumu, heri tumemuombea, wachache wanalaumu, mengi kutoyagundua, ana mengi majukumu, vigumu kuelezea,Rais wa siku zote,tulomuomba Rabuka.10.toka giza litotoro, fika sehemu salama,ujue yalo kasoro, kufika mwanga mapema,utapata mgogoro kwa wasopenda mema, Rais wa siku zote, tulomuomba Rabuka! !!!
Yarabi msimamie,kwa kila alitendalo,mazuri mkirimie,kwa lolote afanyalo, hekima mzidishie, kila saa lipitalo, Rais wa siku zote,tulomuomba Rabuka 5.Saidi mama kipenzi,Sami Suluhu Hassan, Mola ampe mapenzi, ongeza shirikiani, kupitia zote enzi,kutoa yake maoni, Rais wa siku zote tulomuomba Rabuka! !!!

^,

Yarabi msimamie, kwa kila alitendalo, mazuri mkirimie,kwa lolote afanyalo,hekima mzidishie,kila saa lipitalo,Rais wa siku zote tulomuombs

HONGERA RAIS MAGUFULI

Kwanza salamu kwa wote,mi mzima kwa hakika, pongezi zilizo zote, kwa Rais atukuka, Allah muweza wa yote, sifa zinastahika, Rais wa siku zote, tulomuomba rabuka. 2.Hakuna asiyejua, mazuri ayafanyayo, mateso kuyapitia, nchi tuliyozaliwayo, huduma zisosawia, hospitali tuendayo, Rais wa siku zote tulomuomba rabuka. 3.mafisadi walojaa kuneemesha wa kwao, wanyonge waliojaa,ukosefu haki zao, mabaya yaliyojaa, teseka maisha yao, Rais wa siku zote tulomuomba rabuka..KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA, ,KARIBUNI SANA MTAPATA MASHAIRI YANAGUSA KILA NYANJA KUANZIA JUU MPAKA CHINI KAMA PIA NI MSANII UNAHITAJI MASHAIRI KARIBUNI MAONI PIA USHAURI YANARUHUSIWA