6.......Serikali awamu tano, yasema hapa kazi tu, fanyakazi zembe walo, bado wanazihusudu, hiyo subuhi kuchwayo,Simu ndo kama salamu, wewe ndo uitawale, simu isikutawale. ..7....Zimerahisisha vitu, wanawake wanaume, mtu kutana na mtu, mambo yameenda kume, Mawasiliano butu, yamaliza kila tume,Simu usikutawale, wewe ndo uitawale, . 8....Zavunja mpaka ndoa, zachachamua mabosi, zinatia watu doa, sababu ya kuwa ghashi, imani zawaondoa, vichwa havishughulishi, wewe ndo uitawale, simu usikutawale, ..9....Zapoteza ufanisi mambo yanafaitika, wajifanya adinasi, mazuri yanakatika, wanafanya na uasi, mambo yanabadilika,simu isikutawale, wewe ndo uitawale, . 10....Utu wa mtu potea, sababu ya urahisi, watu badilisha namba, simu ndo kiunganishi, ana kwa ana hakuna, moja siku malizana, wewe ndo uitawale, simu isikutawale, ...11....Kama tujuavyo, kuna masika bila mvua, pia zasaidiapo, biashara kuzijua, wengi wapata kipato, tena tumeshuhudia, simu zatusaidia,Sisi ndo twaziharibu, ...12...Wasiliano rahisisha, nje na ndani pia, umoja zimedumisha, wote kuwa familia, mengi imebainisha, mazuri mabaya pia, sisi ndo twaziharibu, simu zatusaidia,...13...Nukuu twazitafuta, ziloandikwa kwa kina, Dalihini kuzipata, mengi yameambatana,walimu kuzifumbata, zote kuzishikamana, simu zatusaidia,Sisi ndo twaziharibu, ...14...Zapunguza pia muda, wa kuanza tafutana, diradira za ukuda, zapungua kwa sana, Hakuna muda poteza, wafanya mambo mengine, sisi ndo twaziharibu, simu zatusaidia.....15.....Hakuna wa kubabaka,ukweli wajulikana, japo wametuletea, ila zinatumbaza, mzazi simpe mwana, ukaona wampenda, Hapo unampoteza, bila mwnywe kujua, ...SHAIRI HILI LIMEISHIA HAPA USIKOSE SHAIRI LINGINE ZURI SANA, ,,,,
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa MwenyeziMungu, lakini pia na kwa wadau wangu wote, ambao wananishauri, na kunipa maoni, kwanza kabisa napenda kuongelea suala la matumizi ya mitandao ya kijamii, limekua tatizo kivipi? naomba tuungane kwa kusoma shairi lifuatalo tuburudike, lakini pia tupate ujumbe kwasababu kama halikugusi wewe moja kwa moja linamgusa ndugu yako au mtu wako wa karibu. ....tuimbe pamoja,,,,1...Whatsup, Facebook, Twitter, insta na napchat, mlahaka vilipata, ghafla ikawa dabali, bila hata ya kusota, wengi walivikumbata, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ..2..Ilianza taratibu, hii teknolojia, dahari ikaharibu, kuja smatifonika, watu wawa kama duku, wawapo mitandaoni, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ...3...zauzwa fulusi ndogo, kila moja amiliki, hata watoto wadogo, zawatia daathari, wanapita kwa mikogo, wazishikapo kwa ari, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ..4...wanafunzi shindwa soma, wabaki kuwa madusa,akili zao zahama,simu zawagusa gusa, wawapo shule ...
Upo vizuriiii
ReplyDelete