SHAIRI HILI NI ZURI SANA LINAONGELEA WAZAZI WA KIDIGITALI NA MALEZI /MAKUZI YA WATOTO, WAZAZI WA SIKU HIZI WAMEJISAHAU SANA KWENYE MALEZI YA WATOTO HII NI HATARI KWA MENGINE TUUNGANE KATIKA SHAIRI HILI, KARIBUNI SANA, ..."""""MTOTO NA MAMA AU BABA WA KIDIGITALI """""1....Mambo yamebadilika,wazazi zama na sasa, Malezi kughafilika, watoto shindwa kuasa, maovu yamefurika, umetuzidi usasa, baba, mama, digitali, mtoto atakuaje? 2....Mama nyonyesha hataki, falaula angejua,Kuja kutahamalaki, mtoto asiyekua, anamkosesha haki, mengine kuyatambua, Mtoto atakuaje? Baba, mama, digitali, ...3....Mtandaoni warusha, sherehe kubwa wafanya, lakini kumnyonyesha, kitu wasichokifanya, mapenzi yasiyokwisha, toto aweze kunyonya,baba, mama, digitali, mtoto atakuaje? 4.....Imani zimewatoka, nguo za wavaa, wajifanya mababaka,elewi yalowajaa, kila siku wanaruka,uzungu usowafaa, mtoto atakuaje? Baba, mama, digital, ..5...Malezi kitu muhimu, msifanye marinara, tuyashike majukumu, tusifanye kama dura, tufanye kama salamu, isiwe ni kama kura, baba mama, digitali, mtoto atakuaje? Usikose muendelezo wa shairi hili, pia usiache kutoa maoni na ushauri...6...Mtoto jama heshima , basi tuikumbatie, wengine wahamahama,machozi tusiwatie, tufanye kama adhama, mazuri tuwapatie, mtoto atakuaje ? Baba, mama, digitali, ..7...Mtoto atakuaje? Baba, mama, digitali, ushauri ulioje, wafanye ilo halali, sifanye kama chiwale, watoto walio Ally, malezi ya siku hizi, yahitaji umakini, 8....sio msikitini, wala sio kanisani, wazazi hawapajui, bize ni mtandaoni, wabidi wawe bai, mazuri usambazani, yahitaji umakini, malezi ya siku hizi, ..9. ....Nalia na marahimu, wao ndo msimamo, mengi wakiyafahamu, maadili yatawemo, hakuna asofahamu,wanawake ndio nguzo, wanawake jitambua , maovu yatapungua, 10.....Gashi ni kujiheshimu,kuanzia utotoni, mazuri kuyakirimu, kuyafanya kama fani, kuyashika majukumu, hadhira si kwa fanani, maovu yatapungua, wanawake jitambua, ..KWA LEO NAISHIA HAPA KESHO NTAENDELEA NA SHAIRI HILI KARIBUNI SANA
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa MwenyeziMungu, lakini pia na kwa wadau wangu wote, ambao wananishauri, na kunipa maoni, kwanza kabisa napenda kuongelea suala la matumizi ya mitandao ya kijamii, limekua tatizo kivipi? naomba tuungane kwa kusoma shairi lifuatalo tuburudike, lakini pia tupate ujumbe kwasababu kama halikugusi wewe moja kwa moja linamgusa ndugu yako au mtu wako wa karibu. ....tuimbe pamoja,,,,1...Whatsup, Facebook, Twitter, insta na napchat, mlahaka vilipata, ghafla ikawa dabali, bila hata ya kusota, wengi walivikumbata, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ..2..Ilianza taratibu, hii teknolojia, dahari ikaharibu, kuja smatifonika, watu wawa kama duku, wawapo mitandaoni, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ...3...zauzwa fulusi ndogo, kila moja amiliki, hata watoto wadogo, zawatia daathari, wanapita kwa mikogo, wazishikapo kwa ari, simu isikutawale, wewe ndo uitawale, ..4...wanafunzi shindwa soma, wabaki kuwa madusa,akili zao zahama,simu zawagusa gusa, wawapo shule ...
Upo vizuri sanaaa
ReplyDeleteNashukuru sana
Delete